Latest News

SPORTS

Liverpool. Liverpool imeendelea kuonyesha ubabe wake kwenye Ligi Kuu England baada ya kuichapa Wolves mabao 2-1 kwenye mechi iliyopigwa Uwanja wa Anfield. Ushindi huu umeifanya Liverpool kuendelea kujidhatiti kileleni ikiwa na pointi 60, saba mbele ya Arsenal inayoshika nafasi ya pili baada ya kila moja kucheza michezo 25.

Luis Diaz ambaye amekuwa kwenye kiwango cha juu kwa siku za hivi karibuni alikuwa wa kwanza kuifungia Liverpool bao katika dakika ya 15 tu ya mchezo baada ya kuyatumia vyema makosa ya mabeki wa Wolves. Dakika saba kabla ya mapumziko Mohamed Salah aliifungia Liverpool bao la pili kwa mkwaju wa penalti na kuifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0, likiwa ni bao la 23 kwa mshambuliaji huyo.

Dakika ya 67, Matheus Cunha alifungia timu yake bao moja hali ambayo ilibadili kabisa mchezo huo baada ya Wolves kupata nguvu na kushambulia kwa nguvu lango la Liverpool ambao walitumia muda mwingi kulinda ushindi wao. Wolves wameendelea kuwa kwenye nafasi mbaya baada ya kuwa katika nafasi ya 17 ikiwa na pointi 19 tu baada ya michezo 25.

EDUCATION

Kamati ya kudumu ya Bunge ya TAMISEMI imeipongeza Halmashauri ya Chamwino Kwa kuonyesha na kusimamia thamani ya fedha katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya elimu katika Halmashauri hiyo. Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Justin Nyamoga ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya elimu ambapo Kamati hiyo ilitembelea katika Shule ya Sekondari Wasichana Manchali na Shule ya Msingi Membe.

“ukipita utaona thamani ya fedha inaonekana katika miradi hii, fedha iliyoletwa inaendana na matokeo tunayoyaona kwahiyo Kamati inawapongeza wote Kwa usimamizi mzuri wa miradi”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe.Festo Dugange, amesema ofisi yake imepokea maelekezo mbalimbali yaliyotolewa na Kamati hiyo na kuyasimamia katika Halmashauri mbalimbali Nchini.

OTHER

PDF NNE LEO: MAELFU YA MAJINA YA WALIMU WALIOITWA KAZINI NA KADA MBALIMBALI LEO FEBRUARY 14, 2025.

Gusa hapa kupata Orodha hiyo

Events

Upcoming Events

No Upcoming Events